SIRI LYRICS- VANESSA MDEE FT BARNABA





Tosa la secret baby
Jamais!

Yooo zane valee baby
Yooo zane valee papaaa

Barnaba
Treni langu la kutongoza limefunga breki
Na kituo ndo wewe (ndo wewe kipenzi)
Sina mengi mimi sio mtoto wa mjini
Nimefundwa jandoni kipenzi

Vanessa Mdee
Hadithi hadithi uongo njoo
Haya nieleze porojo, mi bado mdogo
Hivi ni juzi ulikuja na mauwa (yes)
Kulikuwa na barua ila sikuifungua na na na (why)

Barnaba
Ungesoma ndani (why), ungejua vingi (no)
Vile moyo wangu ulivo jawa na vigingi
Wewe una mume (nampenda) na mi nna mke
Twaweza iba bado wasishituke! (loh)

Vanessa Mdee
Kumbe muhuni
Hapo siwezi kushare penzi nawe
Kasoro yangu nini
Si una mke yule amekosa nini
Oh yeah, ooh oohh!

Barnaba
Kwanza ningekuomba
Kipenzi ukubali
Tutafanya siri ya watu wawili

Vanessa Mdee
Utaniponza kwa jambo hili
Hamnaga siri ya watu wawili

Barnaba
Kama ukikubali
Nitakupa kagari
Na visalary
Utakuwa bonge la sister du

Vanessa Mdee
Alinifunza mama
Niogope wavulana
Nikae mbali
Nyie wabaya sana

Vanessa Mdee
Kwetu nyumbani
Tumekulia kwenye dini mmh
Penda wako nyumbani kwanza
Kisha unipende mimi mmh
(Au uongo baba!)

Barnaba
Aah asante kwa muda wako
Nimependa majibu yako
Hivi nikuulize swali? (niulize nini?)
Anavyo toka mumeo unajua mangapi anafanya?
Ni muhuni (muongo)
niseme nini (muongo)
Kila kitu (muongo)
Maneno yangu hayakuvuna pendo

Vanessa Mdee
Huna jipya (muongo)
Useme nini (muongo)
Maneno yangu (muongo)
Kibaya zaidi mke wako akijua

Vanessa Mdee
Kumbe muhuni
Hapo siwezi kushare penzi nawe
Kasoro yangu nini
Si una mke yule amekosa nini (oh no)
Oh yeah, ooh oohh! (ebo!)

Barnaba
Ukikubali
Nitakupa kagari
Na visalary
Utakuwa bonge la sister du

Vanessa Mdee
Alinifunza mama
Niogope wavulana
Nikae mbali
Nyie wabaya sana

Barnaba
Kwanza ningekuomba
Kipenzi ukubali
Tutafanya siri ya watu wawili

Vanessa Mdee
Utaniponza kwa jambo hili
Hamnaga Siri ya watu wawili

Barnaba
Kama ukikubali
Nitakupa kagari
Na visalary
Utakuwa bonge la sister du

Vanessa Mdee
Aliniifunza mama
Niogope wavulana
Nikae mbali
Nyie wabaya sana
available on Telegram Song Lyrics
Related : SIRI LYRICS- VANESSA MDEE FT BARNABA.